Adsterra netwok

https://www.effectiveperfomancenetwork./iimttpr57?key=9e991b2ffa81bb3fcdaa457a2bdb33ba

Sunday, May 30, 2021

CHANGAMOTO ZA UFUGAJI

    Apo  awali nilielezea ufugaji wa kaa na niliishia kwenye utengenezaji wa chakula cha kaa,napenda twendwe sambamba kutokea tulipoishia,kama wewe aujazisoma basi usijali zote zipo unaweza kuzitafuta kwa kupitia ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝhttps://profileofficial21.blogspot.com 

   Tunahitaji kutambua hakuna jambo lisilo na changamoto,na changamoto KUJITOKEZA ili uweze kuboresha.Ufagaji wa kaa ambao unategemea mazingira ya fukwe ya bahari inapelekea kujitokeza mambo kadhaa!

 Aina ya chakula cha kutengeneza nichokielezea awali๐Ÿ‘ˆ๐Ÿพkinawasaidia kaa kukomaa ndani ya wiki 3-5 wanakua na uzito wa kutosha na wanakua wamejaza nyama yaani wako vema Sana,sasa tuendelee๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA KWENYE                           UFUGAJI WA KAA

1.Upatikanaji wa mbegu *Kaa maji*,ili uzalishaji wa kana wengi uongezeke ni muhimu kuwe na upatikanaji wa kutosha wa kaa maji ili wahifadhiwe kwenye cages kwa muda na wakomae waiingie sokoni.

2.Usafi wa vizimba wa kila siku,changamoto inajitokeza hasa pale unapokua na idadi kubwa ya vizimba vya kuvifanyia usafi,ili usafishe kizimba ni muhimu kaa aliye ndani yake umtoe kwanza ufanye usafi alafu umrejeshee kunahita umakini mkubwa

3.Ukosefu kwa wafanyakazi wenye ujuzi,endapo utakosa watu wenye ujuzi au utaalamu wa ufugaji au wenye uwezo wa kukamata na kumfunga kaa ni tatito kubwa Sana,kwasababu hautoweza kuwavuna wala kuwasafirisha,wafanyakazi wenye utaalamu wanjua namna ya kuwakamata ili wasivunjike na wanaweza kuwafunga vizuri

4.Vifo vya kaa,unapofuga vifo vya kaa vinajitokeza hasa vipindi vya joto,pia mbegu nyingi zinapokua na majeraha wanapelekea vifo kuwa vingi,ushauri unapokusanya mbegu wale kaa wenye majeraha watenganishe cages zao ili iwe lahisi kufagilia maendeleo tao

5.Wizi wa kaa shambani,unapoamua kufuga kaa Basi akikisha unaweka ulinzi kwenye eneo lako,kaa ni mali kilo moja ya kaa mkubwa yapata Tsh 7000-9000/= kwahiyo weka ulinzi endapo mtu atakuibia 12pcs tu ni sawa umepoteza Tsh 100000/=,Weka ulinzi usiku na mchana kaa ni mali Sana.

6.Kukatikakatika kwa miguu,kutokana na mazingira ya usafi kuhamisha hamisha au kung'atana inapelekea kukatika na kua reject endapo kaa amekatika thaman yake ya soko inashuka yapata  Tsh 1500-3000/= na ndio maana unahitaji uwe na watu wenye kujua kukamata na kufunga vizuri

7.Keji kufumuka,endapo vizimba vinakua eneo ambalo linafikiwa zaidi na mawimbi inachangia cages kuhalibika na kaa wanatoka wenyewe kuingia baharini,zingatia unapojenga cages weka eneo ambalo mikoko iko mwanzo wa bahari na shamba liwe nyuma kidogo ya mikoko ili hata kama kunatokea mawimbi yatapozwa na miti ya mikoko iliyo mbele.

8.Kaa kukaa muda mrefu shambani,endapo kaa wanakomaa ni muhimu uwatoe shambani,unapofuga tafuta soko likusaidie kuwauza kwa wakati pindi wanapo tu wanapokamaa ili kuepuka vifo na reject visivyo vya lazima.

NB: Unapofuga nashauri kufuga kaa kuanzia medium 500gm na Large 700gm wa ndio wenye soko kubwa zaidi.

Mada itaendelea.....................!

Saturday, May 29, 2021

MISULI YA BINADAMU

      Baada ya kuangalia mifupa Katika mada ilihopita ๐Ÿ‘ˆ๐Ÿพ na tumejua mfumo wa mifupa ya binadamu.leo tunaendelea ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

      MISULI KATIKA MWILI WA BINADAMU

Misuli ni sehemu ya nyama kwenye mwili.Binadamu ana misuli 600.

Misuli inatabia ya kusinyaa,kurefuka na kulegea.Misuli iliyounganishwa Ncha za mifupa ikisinyaa huifanya mifupa iweze kujongea

Msuli mmoja ukisinyaa huvuta mfupa,na msuli wa pili ukisinyaa unarudisha mfupa mahali ulipokua awali

Msuli mmoja usinyaa ule wa pili kulegea,misuli mingine haikuunganishwa na mifupa mfano๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

A.misuli inayobeba mishipa ya damu kuiwezesha damu kuzunguka mwilini

B.mapafu na moyo hufanya kazi kwasababu ya mjongeo wa misuli Mara kwa mara.

Misuli ya binadamu iko katika sehemu mbili ambayo misuli ya hiari na isiyo ya hiari na iko Kama hivi ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

1.MISULI YA HIARI ni ile ambayo hujongea mara mtu anapoamua kusimama,kukaa na kujongea kuelekea mahala popote.Hi ni misuli ile iliyoshikilia kwenye mifupa.

2.MISURI ISIYO YA HIARI ni ile ambayo husafirisha chakula tumboni Latina njia ya chakula,na ile ya moyo inayosjkuma damu kwenda sehemu nyingine za mwili.

Misuli yote ipo Nje ya mifupa na Ndani ya ngozi,Misuli inasinyaa na kulegea kulingana na kazi inayofanyika.hadi hapo☝๐Ÿพ☝๐Ÿพ☝๐Ÿพ tuko P1,usiache Ku comment kama Una Swali au maoni asante tukutane kwa mada inayo kuja๐Ÿ‘‰๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿค—


Wednesday, May 26, 2021

MIFUPA YA BINADAMU

     MFUMO WA MIFUPA YA BINADAMU

Leo tuangalie mifupa.

     MFUPA ni sehemu ngumu katika mwili wa binadamu ikifuatiwa na misuli.Mifupa na misuli humfanya binadamu atofautiane na  wanyama wengine.

                    KAZI YA MISULI

1.Kuweka mwili katika umbo lake,

2.Kulinda viungo vya mwili ambavyo ni mapafu,ubongo,moyo,macho,masikio na ulimi.

3.Kutengeneza chembe chembe NYEKUNDU za damu

4.Kushikilia misuli

5.Kutengeneza na kuhifadhi UROTO

         MUUNDO WA MFUPA

Mfupa wa binadamu umeundwa na sehehemu kuu mbili ambazo ni SEHEMU YA NJE ni ngumu na SEHEMU YA NDANI iko kama dodoki na imejaa UROTO.

Katika mifupa ya mikono na miguu kuna uroto wa njano,

Kwenye ncha ya mikono na miguu kina uroto Mwaekundu,Uroto mwekundu hutengeneza seli nyekundu za damu,

Gegedu ni sehemu inayozungukwa na kimiminika kinachaisaidia mifupa kujongea,gegedu ni sehemu laini inayovutika kama mpira,

Mifupa imekaa kwa kushikiliwa pamoja mwa nyuzi nyeupe zilizo imara na zinaitwa mikano.

      IDADI YA MIFUPA YA BINADAMU

Mifupa ya binadamu imepangwa mwili mzima.

Binadamu ana jumla ya mifupa 200

MGAWANYIKO WA MIFUPA YA BINADAMU

Binadamu anamafungu manne ya mifupa ambayo ni Mifupa ya fuvu la kichwa,Mifupa ya kiwiliwili,Mifupa ya maungo ya juu na Mifupa ya maungo ya chini.

.Mifupa ya fuvu la kichwa cha binadamu kuna mifupa 22

.Kiwiliwili cha binadamu kina mifupa 58

Kifua kikiwa na mifupa 25,Kidari mfupa 1 na mbavu zisizo harisi sipo 2,

.Mifupa ya uti wa mgongo

Uti wa mgongo wa binadamu una pingili 12,

Uti wa mgongo wa shingo Una pingili 7,

Uti wa mgongo wa njonga Una pingili 5,

Uti wa mgongo wa kiuno Una pingili 5,

Uti wa mgongo wa mkia wa mwanzo Una pingili 4.

.Mifupa ya Maungo ya chini iko 67,

Mifupa iliyo katika nyonga iko 7,

Mifupa iliyo katika kila mguu iko 30,

Fupa LA nyonga kina umbo LA kibakuli ambalo mifupa 2 yenye mifupa 3 kila mmoja.

           Mifupa ya miguuni: Fupa la lama,Maundi,Safu na Vifupa vya kiwiko,kiganja na kidole.

.Mifupa ya maungo ya juu iko mifupa 64 na,

Mifupa ya mkono wa kiganja iko 2×32=64.

Hadi hapo☝๐Ÿพtumeshajifunza kuhusu mifupa ya binadamu,endelelea kufatilia mada zinazokujia mara kwa mara asnte! Tukutane kwenye maada ijayo hivi punde .........๐Ÿ‘‰๐Ÿพ


Tuesday, May 25, 2021

MAANDALIZI YA UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KAA

 VIFAA MUHIMU VYA UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KAA:

.Karoti robo

.Kitunguu maji robot

.Uduvi 1kg & dagaa la kawaida 1kg

.Viazi mviringo robot

.Unga wa ngano nusu

.Unga was sembe 1kg 

.Unga wa mchele 1kg 

.Maji /mafuta kula

.Sufuria 2 kubwa na ndogo 

.Kinu & chujio.

HATUA ZA UTENGENEZAJI๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

    Baada ya kuona ๐Ÿ‘†๐Ÿพvifaa muhimu vya utengenezaji wa chakula cha kaa,sasa tuangalie jinsi ya kukitengeneza๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

1.Chemsha viazi adi viive

2.Saga karoti na vitunguu

3.Lisagwe/litwange dagaa na uduvi

4.Changanya unga wa mchele,sembe & ngano

5.Changanya karoti,vitunguu vilivyisagwa,dagaa & uduvi vizuri hadi vichanganyike

6.Changanya viazi vilivosagwa na mchanganyiko wa sembe ,ngano na mchele,yaani michanganyiko yote unaweka kwenye chombo kimoja

7.Sasa unaweka unga wa ngano,mchele,karoti,vitunguu,viazi,DA ga a na uduvi hadi vichanganyike kwa kutumia mikono kama unakanda ngano

8.Hatua hii weka maji kiasi mithili ya ngano ya chapati na Tia mafuta kidogo Sana

9.Baada ya hapo tengeneza piece ndogondogo za mchanganyiko huo๐Ÿ‘†๐Ÿพ(Vitonge vidogo vidogo)

10.Unamalizia kwa kupasha moto hizo pieces kwa hatua hizi:

A.Bandika maji jikoni yakiwa katika sufuria kubwa,

B.Weka pieces (vitonge) ya vyakula kwenye sufuria ndogo ambayo haina maji,

C.Weka sufuria ndogo yenye chakula piece ndani ya sufuria kubwa yenye maji na ifunikwe na chujio,

D.Weka kwa muda usio pungua dakika 5 baada ya Mani kupata moto,

E.Baada ya kupata moto/joto chakula kitolewe na kianikwe juani hadi kikauke,

F.Kiko tayari kuanza kutumika kulishia kaa.

NB:☝๐ŸพChakula kitawekwa jikoni Kama tu,kimewekwa mafuta lakini kama hakijawekwa mafuta basi utatengeneza vitonge na kuvianika Moja kwa moja Juani.

Hadi hapo tumemakiza utengenezaji wa chakula cha kaa๐Ÿค— tukutane page ijayo๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ


Saturday, May 22, 2021

MAISHA YA SIMBA

 Leo tuangalie maisha ya MFALME WA NYIKA

Simba ni wanyama wanaishi kifamilia zaidi na kusaidiana katika maisha yao ya mbugani,Simba dume anaumbo kubwa zaidi ya majike,simba wanapenda kuishi eneo lenye wanyama wengi kama punda milia,nyumbu nk.

Simba jike anapo zaa watoto anawaficha kwenye vichaka na mapango makubwa kwa muda wa wiki 6 na kuwatoa kuungana na familia ya simba,familia ya simba inamajukumu mawili UWINDAJI & ULINZI.

Uwindaji wa simba unategemea umoja wao na wanapenda kuwinda wanyama wakubwa ili wale na familia yao,ambao wakisha kamata wanakula familia nzima ya simba.

Simba dume anajukumu la ulizi wa familia na kuzalisha,majike yanawaheshimu sana midume na kuwaamini katika pulukushani kwenye ulinzi wao wa familia,na ni mnyama mwenye sauti nzito sana yenye kusikika.

Simba jike ndiye muwindaji mkuu wa familia,anauwezo mkubwa wa kuwinda wanyama wanapenda kukamata wanyama wakubwa mara nyingi wanaweza kua zaidi ya mmoja.Wanakamata shingo wananyonya damu hadi huyo mnyama afe,baada ya kufa familia ya simba huongezeka na kumla huyo mnyama.Midume hutumia nguvu hata kuwafukuza simba wengine ili ale yeye kwanza,simba dume kwenye kula anaubinafsi sana,kutokana na tabia ya simba dume inawafanya Majike kufikia wakati wakikamata mnyama wanamficha na kuchukua familia kama watoto na Simba wengine wanakula haraka kabla midume haijafika maana wataweza kutimuliwa.

Inapofika kipindi cha ukame Wanyama wengi wanahama kutafuta chakula na maji,inapelekea Simba kua kuwa katika kipindi kigumu cha njaa,kinawafanya Simba wale chochote hadi mayai wanapokutananayo,hiki ni kipindi simba anakula hadi mizoga ilioachwa na wanyama wengine Kama chui na dume,duma wanauwezo mkubwa wa mawindo pasipo kutegemea kampani ya mwenzake,anapokamata anakula anapokutwa na simba anafukuzwa hua cha kula cha simba,maisha ya simba yanakua ya njaa sana inafikia kukamata wanyama wadogo wadogo ambao hata hawakidhi matumbo yao na inawafanya midume kupora chakula anakula peke yake hali hiyo inaendelea kwa simba yapata miezi 6.

Utafiti wa wanyama Simba unaeleza simba anayewinda peke yake anakua na maisha magumu zaidi kwa kukosa chakula,lakini Simba wanaowinda wengi kwa pamoja wanapata unafuu wakupata chakula na anayekamata anakula na simba wengine.

Msimu wa mvua wanyama wengi wanarudi maji na chakula vinapatikana,maisha ya wanyama yanaanza kustawi tena haswa simba maana vyakula vyake vimerudi,lakini kutokana na purukushani Simba wanavunjika mikia na wengine wanakatika kabisa,kwa wale simba walio vunjika miguu wanatengwa na simba midume na wanaishia kula mizoga na wengine kufa kwakuso chakula maana awana uwezo tena was kuwinda.

Friday, May 21, 2021

AINA YA CHAKULA CHA KAA

 Unapo fuga kaa na kuwaweka katika vizimba hakikisha unawapatia chakula,kaa wanakula kiasi kidogo cha gm ya chakula.Wanao fugwa huwa ni kaa maji ambao hawajakomaa na unapowaeka kwenye vizimba ili waweze kukomaa na uwavune uuze au uachemshe,kaa Ana we za kukomaa haraka ama kuchelewa kutokana na aina ya chakula unachopewa,na ili kaa wakomae halaka wanahtaji chakula chenye madini joto/chunvi kwa wingi ambacho kitamkomaza ndani ya wiki 3 hadi 4,lakini ukitumia vyenye protein zaidi anaweza kukaa kwenye kizimba kwa muda mrefu zaidi wiki 6 hadi 8.Chakula kinachofaa zaidi ili wakomae haraka dagaadagaa,au chakula maalumu kilichetengeneza ,na vyenye kumfanya awe na uzito zaidi.tรบtaendea kwenye Page nyingine utengenezaji wa chakula cha kaa inakuja๐Ÿ˜ณ๐Ÿ‘‰๐Ÿพ

Thursday, May 20, 2021

KUFUGA KWA KUTUMIA VIZIMBA (CAGES)

 Tuendelee na somo letu,baada ya kuzingatia mambo muhimu ya kuzingatia napenda kuelezea kuhusu ufugaji wa kutumia VIZIMBA,zipo nyingi lakini ufugaji huu nj njia ambayo inasaidia kaa kufikiwa na maji direct kila siku,pia anapata hata muda wa kubadilisha hewa,kwasababu vizimba hujengwa pembezoni mwa fukwe ambapo maji yanauwezo wa kufika na kutoka ,Maji yanapofika vizimba huwa kwenye maji na yanalotoka vizimba vinakua havina maji.Vizimba ni vijumba vidogo vinavyotengenezwa na vijiti au mbao vyenye upana na urefu angalau Mita 1 za mraba,au Una we za kutumia ndoo  zunye matobo unajengea vizuri kwa kutumia kamba imara,kutokana na Vizimba kufunikwa na maji mara kwa mara vinahitaji kamba maalumi zenye kuvumilia maji nashauri kuna kamba maalumu wavuvi hupenda kuzitumia siko kama Sufi ni imara sana na zinadumu kwenye maji yaani zikiloa ndio imara zaidi.baada ya kuandaa vizimba vyako viwe na mfuniko uwe na uwezo wa kufunika na kufunua,sasa unaanza kuweka kaa wako,kila kizimba weka kaa mmoja tu ili wasiweze kuumana  hatimaye kukatana mikono (magandu),na utaanza kuwaekea chakula kaa mmoja Ana weza kula wastani wa gram kumi kwa siku,utawapa kulingana na idadi ya PC za kaa ulizoweka shambani.tukutane mada ijayo๐Ÿ‘‰๐Ÿพ

Wednesday, May 19, 2021

VITU VYA KUZINGATIA KWA UFUGAJI KAA

 ENEO LA KUANZA KUFUGIA KAA,eneo ni sehemu mehimu kabla ya kuanza kufuga kaa,kaa wanapenda zaidi kuishi kwenye maeneo yenye asili ya udongo wa kichanga na mfinyanzi,eneo linaweza likawa pembezoni mwa fukwe ya bahari na inapendeza zaidi eneo liwe limezungukwa na mikoko ili isaidie kupunguza shuluba itokanayo na mawimbi ya bahari.UPATIKANAJI WA MBEGU baada ya kupata eneo angalia je eneo hilo upatikanaji wake wa mbegu ni rahisi ama laah! Mbegu ndio zitakazoweza kuongeza uzalishaji,upatikanaji wa  mbegu wa kaa Maji ata wagumu,kana maji ni kana ambao bado hawajakomaa na hawawezi kuingizwa sokoni lakini Kaa wagumu ambao wamekomaa wako tayari kuuzwa ama kupikwa.USALAMA WA ENEO HUSIKA ni muhimu Sana kwa usalama wa Mali zako isiwe wewe unaongeza hao wanapunguza,unajaza wanamwaga itachelewesha  mafanikio.VITENDEA KAZI kunahajika vifaa malum mfano kamba,kisu,chombo cha kulishia.PIA ENEO NI MUHIMU LIWE NA UPANKANAJI WA HUDUMA ZA JAAMII eneo lolote linahtaji usalama wa kiafya na hata upatikanaji was maji kea matumizi mengine.Tuendelee ukurasa ujao๐Ÿค”๐Ÿ™„

UFUGAJI WA KAA

 Ufugaji wa kaa ni moja ya aina ya ufugaji Jamii ya samaki,kaa pia hufugwa kwa njia nyingi mfano njia ya kizimba,bwawa/kalo nk.Katika ugugaji wa kaa kuna mambo ya kuyazingatia pindi unataka kufuga ambayo ni: ENEO LA KUFUGIA,UPATIKANAJI WA MBEGU,USALAMA WA ENEO,VITENDEA KAZI VYA KUTOSHA,UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA KIJAMII NA UHAKIKA WA SOKO.Kaa ni kitoweo kizuri kilichojaa ladha ya asili,nyama yake ni nyeupe ambayo inaweza kupikwa kama supu style au kutiwa viungo kua mboga,na pindi imetiwa viungo kwa asiyejua anaweza sema mithili ya mayai yaliotiwa viungo.Nyama ya kaa inapatikana baada ya kuchemshwa na kupasuliwa hutolewa nyama iliyo ndani ya mwili wake,ni vigumu kukadilia uwingi au uzito wa nyama ya kaa kea muonekano wake ingawa Kaa mkubwa anauwezekano wa kua na nyama nyingi zaidi ya mdogo.Ili uweze kupata nyama ya Kaa umchemshe kabla aujotoa ma gamba yake kwa maana chemsha mzimamzima adi aive na akiiva magamba yanabadilika rangi ya Karoti/njano na utahisi harufu inayonukia zaidi na utawatoa jikoni na kuwaacha kDa muda kidogo wapoe kabla ya kuanza kuwapasua kutoa nyama,katika kuchemsha zingatia usitie chumvi wenyewe wanajitegemea wanachumvi ya asili.Hadi sasa umeshaa kumfaham kaa tukutane kea page inayofata๐Ÿค”๐Ÿ‘‡๐ŸฝKufafanua mambo ya kuzingatia kea ufugaji wa kaa Kama nilivyoolodhesha☝๐Ÿพawali.

Tuesday, May 18, 2021

KAA (Crabs) na SIFA ZAKE

Kaa ni moja ya jamii ya samaki waishio baharini,kaa ana umbo ambalo liko tofauti na samaki wengine.Kutokana na umbo lake linamfanya pia awe na lifestyle yake,kaa anauwezo mkubwa wa kuogelea kwenye maji pia anaweza kuishi nje ya maji kwa siku kadhaa! lakini kaa anahitaji maji chunvi zaidi.Kumbuka kuna utofauti kati ya KAA wa bahari na KAA wa mto(NGADU),ngadu ni jamii ya kaa lakini hawa wanaishi bajibaridi(hayana chunvi) na pia wa umbo dogo,KAA sasa ni wakubwa wanaishi baharini wana miguu yenye ncha kama itakanyaga inaweza ikakutoboa au kukuchuna.Kaa hana mkia,ila ana miguu,mdomo,macho mithili ya antena ngamba gumu na anamikono miwili mbele ambayo anaitumia kama silaha na kukamatia chakula,mikono yake ni hatari sana inanguvu ni migumu kaatakukamata kwenye ukucha inaweza ikakatika ama ukapata maumivu makali sana.KAA wako dume na jike na wanata,wanataga kwa kuyaachia baharini kwa mfumo wa jely na hufanyiwa urutubishwaji nje hadi watoto kutoka kwenye mayai hayo,unaweza kumjua kaa dume au jike kwa muonekano wa umbo lao,mfano:Kaa jike ana mikono midogo na miyembamba pia anaumbo dogo,lakini Kaa dume anaumbo kubwa,anamikono mikubwa tena minene.Kaa mmoja anaweza kufikia hadi kilo moja na nusu kaa wa uzito huo ambebe mwenye uzoifu maana mikono yake ni hatari sana.Tutaendelea kwa peji inayofuata na MADA ya ufugaji KAA๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

Kitanda free delivery

 @kitandafreedelivery  Piga/SMS/WhatsApp: 0785322941 YANAFANYIKA MALIPO BAADA YA KUFIKISHIWA MZIGO KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM PEKEE, ©Usafi...