Leo tuangalie maisha ya MFALME WA NYIKA
Simba ni wanyama wanaishi kifamilia zaidi na kusaidiana katika maisha yao ya mbugani,Simba dume anaumbo kubwa zaidi ya majike,simba wanapenda kuishi eneo lenye wanyama wengi kama punda milia,nyumbu nk.
Simba jike anapo zaa watoto anawaficha kwenye vichaka na mapango makubwa kwa muda wa wiki 6 na kuwatoa kuungana na familia ya simba,familia ya simba inamajukumu mawili UWINDAJI & ULINZI.
Uwindaji wa simba unategemea umoja wao na wanapenda kuwinda wanyama wakubwa ili wale na familia yao,ambao wakisha kamata wanakula familia nzima ya simba.
Simba dume anajukumu la ulizi wa familia na kuzalisha,majike yanawaheshimu sana midume na kuwaamini katika pulukushani kwenye ulinzi wao wa familia,na ni mnyama mwenye sauti nzito sana yenye kusikika.
Simba jike ndiye muwindaji mkuu wa familia,anauwezo mkubwa wa kuwinda wanyama wanapenda kukamata wanyama wakubwa mara nyingi wanaweza kua zaidi ya mmoja.Wanakamata shingo wananyonya damu hadi huyo mnyama afe,baada ya kufa familia ya simba huongezeka na kumla huyo mnyama.Midume hutumia nguvu hata kuwafukuza simba wengine ili ale yeye kwanza,simba dume kwenye kula anaubinafsi sana,kutokana na tabia ya simba dume inawafanya Majike kufikia wakati wakikamata mnyama wanamficha na kuchukua familia kama watoto na Simba wengine wanakula haraka kabla midume haijafika maana wataweza kutimuliwa.
Inapofika kipindi cha ukame Wanyama wengi wanahama kutafuta chakula na maji,inapelekea Simba kua kuwa katika kipindi kigumu cha njaa,kinawafanya Simba wale chochote hadi mayai wanapokutananayo,hiki ni kipindi simba anakula hadi mizoga ilioachwa na wanyama wengine Kama chui na dume,duma wanauwezo mkubwa wa mawindo pasipo kutegemea kampani ya mwenzake,anapokamata anakula anapokutwa na simba anafukuzwa hua cha kula cha simba,maisha ya simba yanakua ya njaa sana inafikia kukamata wanyama wadogo wadogo ambao hata hawakidhi matumbo yao na inawafanya midume kupora chakula anakula peke yake hali hiyo inaendelea kwa simba yapata miezi 6.
Utafiti wa wanyama Simba unaeleza simba anayewinda peke yake anakua na maisha magumu zaidi kwa kukosa chakula,lakini Simba wanaowinda wengi kwa pamoja wanapata unafuu wakupata chakula na anayekamata anakula na simba wengine.
Msimu wa mvua wanyama wengi wanarudi maji na chakula vinapatikana,maisha ya wanyama yanaanza kustawi tena haswa simba maana vyakula vyake vimerudi,lakini kutokana na purukushani Simba wanavunjika mikia na wengine wanakatika kabisa,kwa wale simba walio vunjika miguu wanatengwa na simba midume na wanaishia kula mizoga na wengine kufa kwakuso chakula maana awana uwezo tena was kuwinda.
Kweli Simba acha aitwe Mfalme,maisha yake yanavutia sana
ReplyDelete