Adsterra netwok

https://www.effectiveperfomancenetwork./iimttpr57?key=9e991b2ffa81bb3fcdaa457a2bdb33ba

Tuesday, May 25, 2021

MAANDALIZI YA UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KAA

 VIFAA MUHIMU VYA UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA KAA:

.Karoti robo

.Kitunguu maji robot

.Uduvi 1kg & dagaa la kawaida 1kg

.Viazi mviringo robot

.Unga wa ngano nusu

.Unga was sembe 1kg 

.Unga wa mchele 1kg 

.Maji /mafuta kula

.Sufuria 2 kubwa na ndogo 

.Kinu & chujio.

HATUA ZA UTENGENEZAJI👇🏽

    Baada ya kuona 👆🏾vifaa muhimu vya utengenezaji wa chakula cha kaa,sasa tuangalie jinsi ya kukitengeneza👇🏽

1.Chemsha viazi adi viive

2.Saga karoti na vitunguu

3.Lisagwe/litwange dagaa na uduvi

4.Changanya unga wa mchele,sembe & ngano

5.Changanya karoti,vitunguu vilivyisagwa,dagaa & uduvi vizuri hadi vichanganyike

6.Changanya viazi vilivosagwa na mchanganyiko wa sembe ,ngano na mchele,yaani michanganyiko yote unaweka kwenye chombo kimoja

7.Sasa unaweka unga wa ngano,mchele,karoti,vitunguu,viazi,DA ga a na uduvi hadi vichanganyike kwa kutumia mikono kama unakanda ngano

8.Hatua hii weka maji kiasi mithili ya ngano ya chapati na Tia mafuta kidogo Sana

9.Baada ya hapo tengeneza piece ndogondogo za mchanganyiko huo👆🏾(Vitonge vidogo vidogo)

10.Unamalizia kwa kupasha moto hizo pieces kwa hatua hizi:

A.Bandika maji jikoni yakiwa katika sufuria kubwa,

B.Weka pieces (vitonge) ya vyakula kwenye sufuria ndogo ambayo haina maji,

C.Weka sufuria ndogo yenye chakula piece ndani ya sufuria kubwa yenye maji na ifunikwe na chujio,

D.Weka kwa muda usio pungua dakika 5 baada ya Mani kupata moto,

E.Baada ya kupata moto/joto chakula kitolewe na kianikwe juani hadi kikauke,

F.Kiko tayari kuanza kutumika kulishia kaa.

NB:☝🏾Chakula kitawekwa jikoni Kama tu,kimewekwa mafuta lakini kama hakijawekwa mafuta basi utatengeneza vitonge na kuvianika Moja kwa moja Juani.

Hadi hapo tumemakiza utengenezaji wa chakula cha kaa🤗 tukutane page ijayo👇🏽


No comments:

Post a Comment

Kitanda free delivery

 @kitandafreedelivery  Piga/SMS/WhatsApp: 0785322941 YANAFANYIKA MALIPO BAADA YA KUFIKISHIWA MZIGO KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM PEKEE, ©Usafi...