MFUMO WA MIFUPA YA BINADAMU
Leo tuangalie mifupa.
MFUPA ni sehemu ngumu katika mwili wa binadamu ikifuatiwa na misuli.Mifupa na misuli humfanya binadamu atofautiane na wanyama wengine.
KAZI YA MISULI
1.Kuweka mwili katika umbo lake,
2.Kulinda viungo vya mwili ambavyo ni mapafu,ubongo,moyo,macho,masikio na ulimi.
3.Kutengeneza chembe chembe NYEKUNDU za damu
4.Kushikilia misuli
5.Kutengeneza na kuhifadhi UROTO
MUUNDO WA MFUPA
Mfupa wa binadamu umeundwa na sehehemu kuu mbili ambazo ni SEHEMU YA NJE ni ngumu na SEHEMU YA NDANI iko kama dodoki na imejaa UROTO.
Katika mifupa ya mikono na miguu kuna uroto wa njano,
Kwenye ncha ya mikono na miguu kina uroto Mwaekundu,Uroto mwekundu hutengeneza seli nyekundu za damu,
Gegedu ni sehemu inayozungukwa na kimiminika kinachaisaidia mifupa kujongea,gegedu ni sehemu laini inayovutika kama mpira,
Mifupa imekaa kwa kushikiliwa pamoja mwa nyuzi nyeupe zilizo imara na zinaitwa mikano.
IDADI YA MIFUPA YA BINADAMU
Mifupa ya binadamu imepangwa mwili mzima.
Binadamu ana jumla ya mifupa 200
MGAWANYIKO WA MIFUPA YA BINADAMU
Binadamu anamafungu manne ya mifupa ambayo ni Mifupa ya fuvu la kichwa,Mifupa ya kiwiliwili,Mifupa ya maungo ya juu na Mifupa ya maungo ya chini.
.Mifupa ya fuvu la kichwa cha binadamu kuna mifupa 22
.Kiwiliwili cha binadamu kina mifupa 58
Kifua kikiwa na mifupa 25,Kidari mfupa 1 na mbavu zisizo harisi sipo 2,
.Mifupa ya uti wa mgongo
Uti wa mgongo wa binadamu una pingili 12,
Uti wa mgongo wa shingo Una pingili 7,
Uti wa mgongo wa njonga Una pingili 5,
Uti wa mgongo wa kiuno Una pingili 5,
Uti wa mgongo wa mkia wa mwanzo Una pingili 4.
.Mifupa ya Maungo ya chini iko 67,
Mifupa iliyo katika nyonga iko 7,
Mifupa iliyo katika kila mguu iko 30,
Fupa LA nyonga kina umbo LA kibakuli ambalo mifupa 2 yenye mifupa 3 kila mmoja.
Mifupa ya miguuni: Fupa la lama,Maundi,Safu na Vifupa vya kiwiko,kiganja na kidole.
.Mifupa ya maungo ya juu iko mifupa 64 na,
Mifupa ya mkono wa kiganja iko 2×32=64.
Hadi hapo☝🏾tumeshajifunza kuhusu mifupa ya binadamu,endelelea kufatilia mada zinazokujia mara kwa mara asnte! Tukutane kwenye maada ijayo hivi punde .........👉🏾
No comments:
Post a Comment